Tarime Girls Secondary School ni shule pekee ya wasichana ya Bweni na Kutwa iliyopo Tarime Mjini. Shule ina Mazingira mazuri na ya
kisasa ambayo ni rafiki kwa wanafunzi wa kike.
Shule ina maabara za kisasa kabisa kwa masomo ya Sayansi,
Kompyuta, pamoja na Maktaba za kisasa zenye vitabu vyote kwa masomo ya
Sekondari na yenye kutosheleza mahitaji.
Ikitumia walimu wenye ustadi na weledi mkubwa wa malezi na
taaluma, shule ya Sekondari ya Wasichana Tarime Imedhamiria kufanya
mapinduzi yakitaaluma kwa watoto wa kike kwa masomo ya sayansi.
Mazingira ya shule ni mazuri sana kwa kutolea na kupokea
taaluma na malezi ikiwa na miundombinu yote ambayo ni rafiki kwa
wanafunzi kiafya na kiakili.
Shule ya Wasichana Tarime Inapokea wanafunzi wa vidato vyote kuanzia kidato cha Kwanza hadi kidato cha Nne. Tumelenga kufanya mapinduzi ya kukuza taaluma kwa watoto wa kike na kutoa malezi bora.